Ojuku Abraham
SINTOFAHAMU! Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD sasa upo njia panda kuhusu ujio wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayesemwa kutaka kutimka kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Prof. Ibrahim lipumba.
“Kuna vikao vingi ndani ya vyama hivyo kiasi kwamba wameshindwa
kumtaja mgombea wao ili kusubiri kwanza wajue hatima ya Lowassa.
Inadaiwa kuwa Chadema imegawanyika, kwani baadhi ya vigogo wanamtaka
kada huyo wa CCM na wengine wanapinga, CUF wanamtaka hata sasa hivi.
Ninachoweza kukuambia ni kwamba ndani ya Ukawa, hali ni tete,
haieleweki,” kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya umoja huo.
Licha ya viongozi wakuu, chanzo hicho kilidai kuwa hata makada wa kawaida wa Chadema, chama kinachodaiwa kuwa ndiyo lengo la Lowassa, wamegawanyika, kwani wapo wanaomuona kama mwenye mtaji mkubwa kisiasa, huku wengine wakimuona ni doa litakalowapa tabu kuliondoa.
James Mbatia.
Shinikizo la Lowassa linatokana na ukweli kuwa kwa muda mfupi tangu
jina lake liondolewe na Kamati ya Maadili ya CCM kiasi cha
kutowasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu, makundi mbalimbali ya makada
wamejiengua kutoka chama tawala na kujiunga na Chadema, wakiwemo zaidi
ya madiwani kumi na nne na wenye viti wa vijiji wilayani Monduli.
Akizungumzia kuhusu uwezekano wa Lowassa kujiunga na Chadema, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema kilichopo ni uvumi tu ambao hata wao wamekuwa wakiusikia hivyo hana cha kuzungumzia.
SINTOFAHAMU! Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD sasa upo njia panda kuhusu ujio wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayesemwa kutaka kutimka kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Willibrord Slaa.
Habari kutoka ndani ya vyama hivyo zinasema, tangu kukatwa kwa
Lowassa katika kuwania kwake kuteuliwa kuwa mgombea urais, kumekuwa na
shinikizo kubwa kutoka kwa watu mbalimbali, wanaotaka kada huyo wa chama
tawala anayetajwa kuwa na wafuasi wengi ajiunge na Chadema, ili awanie
nafasi hiyo kwa tiketi ya Ukawa.Licha ya viongozi wakuu, chanzo hicho kilidai kuwa hata makada wa kawaida wa Chadema, chama kinachodaiwa kuwa ndiyo lengo la Lowassa, wamegawanyika, kwani wapo wanaomuona kama mwenye mtaji mkubwa kisiasa, huku wengine wakimuona ni doa litakalowapa tabu kuliondoa.
Akizungumzia kuhusu uwezekano wa Lowassa kujiunga na Chadema, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema kilichopo ni uvumi tu ambao hata wao wamekuwa wakiusikia hivyo hana cha kuzungumzia.
0 comments:
Post a Comment