Imelda Mtema
MSANII zao la Kundi la Sanaa la
Kaole, Mwasiti Mohamed ‘Sishi’ zimeanikwa katika mtandao wa kijamii wa
Instagram zikimuonesha wakati akijifungua akiwa kwenye uchungu mkali.
Sishi ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa,
katika picha hizo alionekana kusaidiwa na mama aliyejulikana kwa jina la
Bi. Rukia, ambaye ndiye aliyempeleka nchini humo, huku mashabiki
walioziona picha hizo baadhi wakimuonea huruma huku wengine
wakishangazwa na kitendo hicho wakidai hakikuwa cha kimaadili.
Gazeti hili lilipowasiliana na Bi. Rukia
kwa njia ya mtandao wa WhatsApp alisema; “Mbona hakuna cha ajabu
jamani? Ile ni kumbukumbu tu na huku ni vitu vya kawaida mno, sasa watu
wakichukulia kama ishu kubwa mimi nitashangaa sana kwa kweli.”
0 comments:
Post a Comment