Dustan Shekidele, Morogoro
HAPATOSHI! Vita kali ya kugombea
ubunge imezuka katika familia ya Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kufuatia
watoto wake wawili, Lulu na Sitti Abbasi Mtemvu ambao kwa pamoja
wamechukua fomu ya kugombea ubunge viti maalum kupitia kundi la umoja wa
Vijana (UVCCM) Mkoa wa Morogoro.
Watoto hao wazaliwa wa mkoani Morogoro
waliochangia baba, kwa nyakati tofauti wiki iliyopita walitinga ofisi za
UVCCM Mkoa na kuchukua fomu hizo kimyakimya.
Mashuhuda wa tukio hilo walipenyeza
ubuyu kuwa Lulu ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua fomu hiyo na siku
iliyofuata Sitti aliyeongozana na mama yake mzazi Mariam Mtemvu
walitinga kwenye ofisi hizo na kuchukua fomu hiyo huku mama yake akibeba
jukumu la kupiga picha za tukio hilo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Mkoa wa
Morogoro, lgnas Said Kinywa alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kudai
kuwa kigezo kikuu cha nafasi hiyo ni kwa mwanachama kuwa na kadi na
kutozidi umri wa miaka 30.
Lulu anayeishi maeneo ya Kiwanja cha
Ndege alithibitisha kuchukua fomu na mdogo wake, akidai ni demokrasia
mpya katika familia yao, lakini Sitti aliyeachia ngazi ya umalkia wa
urembo nchini (mwaka 2014) kwa kashfa ya kudanganya umri hakupatikana
kupitia simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment